Mwanafunzi aliyemuua mama yake ili asijue kufukuwa kwake chuo, Ahukumiwa

Mwanafunzi aliyemuua mama yake ili asijue kufukuwa kwake chuo, Ahukumiwa

Aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mount Union, kilichopo Ohio, Sydney Powell, ahukumiwa kifungo cha maisha gerezani baada ya kukutwa na hatia ya kumuua mama yake kwa kumchoma visu ili asijue kuhusu kufukuzwa kwake chuo.

Inaelezwa kuwa Sydney mwaka 2020 akiwa na miaka 19 alifukuzwa chuo hakutaka mama yake afahamu, ndipo alichukua uamuzi wa kumpiga kichwani na sufuria, kisha kumchoma visu zaidi ya 30 shingoni, ili mama huyo asifahamu kuwa amefukuzwa chuo.

Hata hivyo baada ya tukio hilo mama huyo alifariki dunia akiwa hospitali kutokana na majeraha aliyopata, upande wa utetezi walidai kuwa binti huyo alifanya tukio hilo bila kujitambua kwani ana dalili za ugonjwa wa akili.

Lakini upande wa mahakama haukuridhika na utetezi huo ndipo ukatoa hukumu ya kifungo cha maisha kwa binti huyo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags