Mwana FA atamba hakuna msanii wa hip-hop anayemzidi kuandika

Mwana FA atamba hakuna msanii wa hip-hop anayemzidi kuandika

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuna (Mwana FA) amesema kuwa bado hakuna msanii wa miondoko ya Hip Hop aliyeweza kuchukua nafasi yake kwenye uandishi wa mashairi ya muziki huo.

“Mimi ni Shaban Robert wa kizazi hiki najua kuchana, watu wanaandika hivi sasa lakini mimi najua sana” ameongeza FA.

Mwana FA ameyasema hayo akizungumza na vijana katika uzinduzi wa kampeni ya TK MOVEMENT leo Jumamosi, Mei 25, 2025, ambapo amesema haijalishi vijana wamepitia au wanapitia magumu kiasi gani lakini wafungue macho kuangalia walilokuja kulifanya duniani, na watapata namna ya kufikia lengo la kuishi kwao.

“Hadithi ya maisha yangu inafahamika na wengi mara zote nataka kukumbukwa kama Mwalimu, na sio mwalimu wa kushika chaki bali ni Mwalimu kwa maisha ambayo nimeishi na kuyapitia mpaka hapa nilipo” ameongeza.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags