Mwamuzi adondoka uwanjani, Sababu joto kali

Mwamuzi adondoka uwanjani, Sababu joto kali

Katika michuano ya Copa America inayoendelea nchini Marekani, imeripotiwa kuwa mwamuzi msaidizi #HumbertoPanjoj aliyekuwa akichezea ‘mechi’ ya Peru na Canada amedondoka uwanjani kutokana na kuzidiwa na joto kali.

Mwamuzi huyo alidondoka dakika za mwisho za kipindi cha kwanza katika mchezo huo uliopigwa jana kwenye dimba la Children's Mercy Park.

Kwa mujibu wa tovuti ya The Sun News imeeleza kuwa baada ya kudondoka alitolewa na kupatia huduma ya kwanza na mpaka sasa bado haijafahamika hali yake inavyoendelea.

Hata hivyo inadaiwa kuwa Joto limekuwa kali sana nchini humo na kwa siku ya jana katika uwanja huo vipimo vilisoma ni nyuzi joto 38.

Wachezaji wa Canada wameonesha wasi wasi wa usalama wao kutokana na hali ya joto kwa sababu wamekuwa wakicheza ‘mechi’ muda ambao jua bado linawaka.

Mmoja ya wachezaji ambaye ni beki, Alistair Johnston amesema ni mazingira ambayo hawatamani hata kukutana na wapinzani wao, hivyo ametaka wabadilishiwe muda wakuingia uwanjani.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags