Mwamahawa Ally astaafu kuimba taarabu rasmi

Mwamahawa Ally astaafu kuimba taarabu rasmi

MWANAHAWA ALLY ASTAAFU KUIMBA TAARABU RASMI

Mkongwe wa muziki wa Taarabu Mwanahawa Ally amestaafu kuimba muziki huo baada ya kuimba kwa zaidi ya miaka 58.

Sherehe hiyo ya kumuaga ilifanyika usiku wa kuamkia leo Septemba 29,2024 Leders Clup ikipewe jina la ‘Asante Mwanahawa’ ambapo mgeni rasmi alikuwa mtoto wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Mhe. Wanu Hafidhi Ameir.

Mkali huyo aliyewahi kutamba na taarabu ya ‘Roho Mbaya’ wakati wa kuagwa kwake alitoa burudani ya mwisho kwa mashabiki ambao walibahatika kufika katika ukumbi huo.

Mwanamuziki huyo amekuwa katika tasnia hiyo kwa muda mrefu ambapo alifanikiwa kuimba katika makundi kadhaa kutoka Dar es salaam na Zanzibar yakiwemo Jahazi Modern Taarab, East Africa Melody na mengineyo.

Utakumbuka kuwa taarifa ya kustaafu kwakwe ilitangazwa mwezi Agosti mwaka huu na Zamaradi Mketema huku sababu kubwa ya kustaafu kwake ikitajwa kuwa ni maradhi yanayo msumbua.

Mwamahawa Ally amewahi kutamba na nyimbo Mwanamke Hulka, Roho Mbaya, Jitoe kimasomaso, Aliyeniumba Hajanikosea, Viumbe Wazito, Mambo Iko Huku na nyinginezo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post