Mwaka wa kwanza chuoni ndo wakufanya maamuzi

Mwaka wa kwanza chuoni ndo wakufanya maamuzi

Hahahaha! Make hapa kwanza ncheke maana sijui niseme vinachekesha au laah! Haya wale watu wangu wa segment yetu ya unicorner leo nimeona nikusogezee mada hiyo ambayo itakuamsha katika usingizi huo uliolala.

Hivi ushawahi kuachana na course usioipenda na kwenda kwenye course unayoipenda, yeeah! Yote yanawezekana haya niwewe tu kufanya maamuzi yaliyo sahihi.

Watu wengi wa bongo tumekuwa wagumu sana kuwaamini wabongo wenzetu ni kwa vile tuu tumeendekeza utani sana kuliko jambo lolote, tumeskia stori nyingi kuhusu watu kukurupuka kuchagua course na mwishoe kusoma kitu ambacho hakua na matarajio nacho.

Mfano mkubwa kuna baadhi ya marafiki zangu tulioingia mwaka wa kwanza chuo semister ile ya kwanza tu ilipoisha na wao hawakurudi tena kutokana na machaguo yao hayakuwa sahihi kabisa, so hata wewe mwanafunzi uliokuwepo chuo unaweza kulifanya hili niwewe kujitathmini na kile ukifanyacho tuu.

Sasa leo nakusogezea baadhi ya watu/wanafunzi waanaosoma nje ambao walimefanikiwa katika kubadilisha course najua ningetumia wanafunzi wenzetu wa bongo kuna baadhi ya watu wasingewaamini, kwa leo nakusogezea mwanadada mmoja so ungana nami mwanzo mpaka mwisho kuwafahamu mwanadada huyu mwanafunzi aliobadili course.

Kama nilivyokueleza hapo juu kuwa mwaka wa kwanza chuoni ndo mwaka wako wa kufanya maamuzi ambayo yatabeba maisha yako yote, na huyu ninaokusogezea hapa alifanya maamuzi akiwa mwaka wa kwanza…

Lily Carson


Mwaka wangu wa kwanza kutoka chuo nilicho kuwa nimesoma niliamua kusoma sheria. Lakini niligundua haraka kwamba haikuwa kile nilichotakiwa kufanya na nikaamua kuchukua mapumziko ya mwaka mmoja.

Kwasasa Mimi ni dansi na kwa hivyo nilienda kucheza dansi huko Los Angeles miezi miwili ilipopita ndipo nilipogundua tena mapenzi yangu na kitu ninachokipendelea Zaidi ni densi hivyo nikaamua kusomea kile nikipendacho.

Mwanzoni nilihisi woga kwasababu ilikuwa mara yangu ya pili kuanza chuo kikuu chingine. Nakumbuka nilifikiria ikiwa hii haitafanikiwa, basi sijui nitafanya nini tena.

Lakini woga na wasiwasi wangu wote uliondoka nilipoingia katika darasa hilo siku ya kwanza yaami Kulikuwa na hisia za kifamilia yaani kama niko nyumbani ilinisaidia kujuana na wanafunzi wangu haraka na hapo maisha yangu mapya ndipo yalipoanzia.

Ushauri wangu kwa wanafunzi wapya ni kuzungumza na watu katika darasa lako  haraka unapounda uhusiano huo na wanafunzi wenzako, itakuwa rahisi kwako.

Wanafunzi wenzako ndio wanaofanya uone course unayosemea kuwa ya kufurahisha na kukusaidia kutokukosa kipindi kila siku maana hii pia inaweza kuja kuwa sababu yaw ewe kuona unachokisoma hakieleweki, kwasasa najiona mwenye bahati sana kuwa na nafasi hiyo ya pili na sasa ninasoma kile ninachopenda.

Naona kama tumalize kidizaini hii, kama tulivyo ongea hapo juu na mmeona maelezo ya mwanadada Lily so nawewe haujachelewa uwanja ni wako sasa kufanya maamuzi yaliyosahihi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags