Museveni akutwa na Corona

Museveni akutwa na Corona

Wizara ya Afya kutoka nchini Uganda imeeleza kuwa rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni akutwa na maambukizi ya Uviko-19 ambapo alianza kupata dalili za homa na mafua makali ingawa hali yake sio mbaya na anaendelea na kazi kama kawaida huku akipata matibabu.

Juni 7, 2023 baada ya kutoa hotuba kwa Taifa katika viwanja vya Bunge, Museveni alidokeza kuwa huenda alikuwa ameambukizwa Corona baada ya kuhisi baridi kidogo, na kumfanya aombe kufanyiwa vipimo.

Aidha katika kilele cha janga hilo, Uganda ilikuwa na sheria kali za kuzuia na kudhibiti maambukizi zikiwemo amri za kutotoka nje, kufungwa kwa biashara, shule na mipaka ya nchi hiyo, na iliweza kuondoa  vikwazo vyote Februari 2022.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags