Museveni ajitenga na uvumi wa kifo chake

Museveni ajitenga na uvumi wa kifo chake

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameweka ujumbe kwenye mtandao wa Twitter na kusema kuwa bado anajitenga kufuatia uvumi wa mitandao ya kijamii kwamba amefariki kutokana na Covid-19.

Rais huyo alipimwa na kukutwa na Covid-19 mnamo tarehe 7 Juni na akasema siku iliyofuata kwamba alikuwa akichukua likizo ya lazima.

“Leo ni siku ya tano ya hali yangu ya corona jana usiku, nililala vizuri sana hadi saa kumi za usiku”alisema Museveni.

Aidha aliwataka waganda kwenda kupata chanjo ya Covid na ile ya nyongeza, haswa kwa wazee.

Mbali na hayo shirika la Afya ulimwenguni lilitangaza mwezi uliopita kwamba Covid haikuwa tena dharula ya tatizo la afya ulimwengu, lakini ilionya kwamba virusi hivyo vitaendelea kubadilika.

Chanzo BBC






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags