Muonekano mzuri wa ngozi kwa wanaume

Muonekano mzuri wa ngozi kwa wanaume

Hello guys!! Acha nikusalimu kwa jina la fashion mtu wangu tunakutana tena another weekend ili tuweze kupashana mambo ya Fashion na tuna hakikisha haupitwi na kitu ngojea tuone leo kuna nini kwenye kapu letu.

Leo katika Fashion tumeingia kwa undani zaidi katika maswala ya urembo, tumekusogezea jinsi ya kuwa na muonekano mzuri wa ngozi kwa wanaume.

Hivi unajua muonekano mzuri unaanzia kwenye urembo na hapo ndio tunapata Fashion ilio kamili wengi wetu hatujui hili suala halifatiliwi hasa kwa wanaume wamekuwa ni watu wasio jijali nitakufafanulia leo twende kazi sasa.

Ngozi ya mwanadamu ni sehemu ya mwili ambayo unahitaji matunzo kama zilivyo nyingine ili iweze kuwa na afya na mvuto wake wa asili.

Tofauti na hapo mtu asipotunza ngozi yako inaweza kukufanya kupoteza mvuto wako na hata kupata magonjwa ya ngozi kama vile chunusi, mapele ukurutu na mengineyo.

Kumekuwa na dhana miongoni mwa wanajamii kuwa masuala yanayohusu utunzaji wa ngozi yanawahusu wanawake pekee hivyo kuwafanya kujiweka kando katika masuala hayo.

Hilo linadhihirishwa na Albert Changarawe mkazi wa Tandale jijini Dar es Salaam ambaye anasema kuwa afahamu njia yeyote ya kutunza ngozi yake zaidi ya kuoga kwa maji safi pamoja na kupaka mafuta.

“Hayo masuala mara nyingi hufanywa na wanawake kwa sababu ndio wanapenda masuala ya urembo” alinasema Albet.

Hatukuishia hapo tukaelekea kwa upande wa Hassan Hassan mkazi wa Buguruni jijini Dar es Salaam anasema imeshazoeleka katika jamii kuwa suala la kuhangaikia ngozi ni la mwanamke pekee anasema.

“Mara nyingi baadhi ya wanaume ufanya uwamuzi wa kuanza kuzitunza ngozi zao hadi pale wanapopata changamoto ya ngozi kama vile kuwashwa, kupata mapele na nyinginezo”alinasema kijana huyo.

Hata hivyo wataalamu wa masuala ya ngozi na urembo wanaeleza kuwa wanaume wana wajibu wa kujijali katika sekta zote za urembo na fashion katika masuala ya utunzaji wa ngozi zao kama wanavyofanya wanawake kwani muonekano mzuri usoni kwa wanaume husababishwa na kujali vizuri ngozi na uso kwa ujumla.

Akizungumza na Mwananchi Scoop mtaalamu wa masuala ya urembo na fashion kutoka Crystal Wedding Accessories, Irene Shamge anasema kuwa ili mwanaume aweze kuwa na ngozi nzuri anapaswa kuwa na tabia ya kunawa uso mara kwa mara ili kuondoa takataka, vumbi pamoja na jasho lililoingia katika ngozi kutokana na mizunguko ya siku nzima.

“Vumbi, jasho na hata takataka zingine katika ngozi haswa ya uso zikikaa kwa muda mrefu huweza kusababisha changamoto ya kupata chunusi, mapele na hata kuharibika kwa ngozi na hauwezi kwenda na fashion” alinasema mwanamitindo huyo.

Irene anasema kuwa matumizi ya visafisha uso (facial cleanser) kila asubuhi ni muhimu pia kwa wanaume kwani husaidia ngozi zao kutoa uchafu na mafuta yaliyozidi kwenye ngozi na kuacha ngozi yako ikiwa nzuri kabisa.

Pia kufanya singo (scrub) mara moja au mbili kwa wiki kwani itasaidia kuondoa seli zilizokufa kwenye ngozi na kuifanya ngozi kuwa yenye kuvutia na huleta muonekano mzuri.

“Pia ni vyema baada ya kunyoa ndevu ni vyema kutumia mafuta yatakayosaidia kuepusha na kupata vipele na kwa wale wanaofuga kwajili ya fashion ni vizuri kuzitunza ili kuweza kuwa na muonekano mzuri” alinasema Irene.

Vilevile anasema ni muhimu kutumia mafuta au losheni inayoendana na ngozi ya mwili wako ili kulainisha ngozi yako.

Anaongezea kuwa ni muhimu kunywa maji ya kutosha kwani husaidia kuzuia kuondoa uchafu na mabaki ya uchafu mwilini kwa njia ya jasho na mkojo pamoja na kupunguza uchovu wa mwili.

“Mtu mzima anashauriwa kunywa maji safi na salama kiasi cha lita moja na nusu kwa siku au glasi nane kwa siku”

Nikikwambiaga fashion imebeba vitu vingi na ni maisha ya kila siku kama kwenye Afya, urembo na muonekano mzuri hapa hauwezi ukabisha mwanetu muonekano wa mtu unazingatia hadi mtindo wake wa kawaida katika mwili wako kina bebwa na muonekano mwamba nikwambie tu sisi tutaendelea kukupa za ndani katika kapu la fashion okay till next weekend my fans.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags