Muna love:  Mtu anaweza kunuiona kama chizi ila Mungu ananielewa

Muna love: Mtu anaweza kunuiona kama chizi ila Mungu ananielewa

Moja katii ya stori ambayo iko mitandaoni ni hii hapa ambapo Muna love ameamua kuwajibu walimwengu kuhusu mambo mbalimbali wanayomdhania kutoka kwenye ukurasa wake wa  Instagram ameandika ujumbe huu hapa.

 ''Kuna wakati mtu anaweza kuniona kama chizi ila Mungu ananielewa kwakua ananijua na pia anajua patano langu mimi na yeye so nafocus na MUNGU wangu.

Hakuna binadamu asiekosea huku duniani hata watumishi wa Mungu wanakosea kwakua ni binadamu tu , Lakini Mungu anawainua tena ili kutulisha Neno .

Mimi huyu ata kama unipendi, unanichukia tu au vile unavyoamini kwa kusikia habari yangu na kujivalisha chuki juu yangu namuomba Mungu akusamehe akujaze baraka uishi maisha marefu ili unione mimi kama Ushuhuda wako na siku moja utashuhudia popote

Ilo swala la kukoment kila siku kua mimi nimemuuaa mwanangu saivi nakula raha sina muda wakujielezea Mungu ananijua na unaeamini amini tu na msizani ndo fimbo ya kunirudisha nyuma nilie machozi sasa basi.

Mimi ni ushuhuda unaoishi , mapito yangu mengi yalipita mbele yenu na hata baadhi mlijua sitaishi ntakufa , ila kuna muweza wa yote aliye hai alinikumbatia huyu ni yesu

najivunia Yesu kunitumia ,

kuniadhibu
kunisamehe na kunilinda na kunishindia vita zangu.

Ninatamani siku moja na wewe uwe na kitu kinaitwa IMANI , neno dogo ila ni mwisho wa matatizo ''.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags