Muigizaji Bruce akutwa na  matatizo ya akili

Muigizaji Bruce akutwa na matatizo ya akili

Familia ya Muigizaji maarufu kutoka nchini marekani Bruce Willis mwenye umri wa miaka 67 imeeleza kuwa mwamba huyo anashida ya akili inayofahamika kwa jina la “Frontotemporal”

Aligunduliwa kuwa na aphasia  ambayo husababisha matatizo ya kuzungumza  katika majira ya joto mwaka jana, lakini hii imeendelea na amepewa uchunguzi maalumu.

Familia iliendelea kusema shida ya akili ya frontotemporal ni aina ya kawaida ya matatizo ya kiakili yanayowaathiri watu walio na umri wa chini ya miaka 60.

“Mpaka sasa hakuna matibabu ya ugonjwa huo, tatizo ambalo tunatumai linaweza kutatuliwa miaka ijayo”

Willis alipata umaarufu katika miaka ya1980 na 90 baada ya kuigiza katika filamu maarufu kama vile Die Hard, The Sixth Sense, Armageddon na Pulp Fiction.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post