Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa kushirikiana na Hospitali ya Queen Elizabeth ya nchini Uingereza itafanya kambi Maalumu ya upasuaji wa kuweka nyonga na magoti bandia kwa wagonjwa wenye changamoto za maradhi hayo mwishoni mwa mwezi huu.
Akielezea kambi hiyo, Daktari Bingwa wa Upasuaji Mifupa, Nyonga na Magoti, Dkt. Shilekirwa Makira amesema wagonjwa watakaonufaika na huduma hizo ni pamoja na wenye matatizo ya nyonga zilizosagika zenye maumivu makali na magoti yaliyosagika.
Dkt. Makira ameongeza kuwa watu wenye changamoto hizo watabadilishiwa kwa kuwekewa nyonga na magoti bandia kitu kitakachowafanya waondokane na maumivu wanayoyapata kabla ya nyonga zao kubadilishwa.
“Tungependa watu wajitokeze na kujisajili mapema kabla ya tarehe 27.11.2023 ili hospitali iweze kufanya maandalizi stahiki ikiwemo pamoja na kufanya vipimo vya awali ambayo ni muhimu kabla ya kufanya upasuaji huu” amesisitiza Dkt. Makira
Dkt. Makira amefafanua kuwa kwa wale waliojiunga na Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya, mfuko unagharimia zaidi ya asilimia 90, pia bima zingine zinagharimia matibabu haya hivyo wasisite kujitokeza kuchangamkia fursa hii adhimu.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi
Leave a Reply