Mtoto wa Mugabe akamatwa

Mtoto wa Mugabe akamatwa

Mtoto wa Rais wa zamani Nchini Zimbabwe Robert Mugabe anashikiliwa na polisi katika mji mkuu wa Harare, kwa madai ya kuhusika katika uharibifu wa magari wakati wa tafrija mwishoni mwa wiki.

Gazeti la serikali la Herald linaripoti kuwa Robert Mugabe Junior huenda akashtakiwa kwa uharibifu mbaya wa mali kimakusudi, Licha ya shutuma hizo yeye na mawakili wake bado hawajatoa maoni yao kuhusu ripoti hiyo.

Mugabe Junior ni mtoto wa pili wa marehemu Mugabe na mjane wake, Grace.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags