Mtoto wa miaka 8 aiba gari kwa kutumia silaha

Mtoto wa miaka 8 aiba gari kwa kutumia silaha

Mtoto wa miaka nane kutoka Alabama nchini Marekani amekamatwa na Polisi baada ya kuiba gari kwa kutumia bunduki na kuanza kukimbizana na Polisi.

Kwa mujibu wa chombo cha habari NBC15 News imeeleza kuwa, Polisi walipokea taarifa ya wizi wa gari mapema wiki hii ambapo kufuatia msako mkali na kukimbizana barabarani, Mtoto huyo aliishia kuligonga gari jingine na kukimbia kwa miguu.

Lakini baadaye alikamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi na kushtakiwa kwa wizi wa daraja la kwanza, kujaribu kuwatoroka Polisi pamoja na kumiliki silaha.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags