Mtoto wa Diddy amvaa 50 Cent

Mtoto wa Diddy amvaa 50 Cent

Baada ya siku ya juzi mawakili wa mkali wa Hip-hop kutoka Marekani Diddy kuomba mahakama kufuta baadhi ya kesi kutokana na kesi hizo kuwa za uongo, kijana wa Combs, King Combs yeye ameamua kudili na waliomgeuka baba yake wakati wa kesi zinazomzunguka.

King siku ya Jana, Mei 13, 2024  ameachia ngoma akiwachana wale wote waliomgeuka baba yake wakati anaandamwa na kesi za unyanyasaji wa kingono ambapo alianza na Rapa 50 Cent ambaye amekuwa akimuandama Diddy tangu afunguliwe kesi na aliyekuwa mpenzi wake Cassie mwaka 2023.

Hata hivyo kupitia ngoma hiyo pia aligusia kidogo kuhusu polisi walivyo vamia nyumba yao iliyopo Miami akidai kuwa polisi ni kama hawakuja kufanya msako bali waliwavamia kama nyumba yao ni yawauza madawa.

Ikumbukwe kuwa Machi 25, 2024 makazi ya nyota wa muziki wa hip-hop, Sean "Diddy" Combs, ya Los Angeles na Miami yalifanyiwa upekuzi na Mawakala wa Usalama wa Taifa kama sehemu ya uchunguzi wa serikali kuhusu madai ya biashara ya ngono yanayomhusisha msanii huyo huku watoto wake wa kiume wakikamata na polisi.

Aidha kutokana na ngoma hiyo 50 hakulikalia kimya suala hilo ambapo kupitia ukurasa wake wa instagram alieleza kuwa kwa sasa anahofia maisha yake kutokana na vitu alivyoviimba King Combs huku akiwaomba wasimdhuru.

Diddy amekuwa akiandamwa na kesi za unyanyasaji wa kingono tangu mwaka jana 2023, kati ya waliowahi kumtuhumu ni aliyekuwa mpenzi wake Cassie, pia mtoto huyo wa Diddy, King naye mwanzoni kwa mwezi Aprili alishitakiwa kwa unyanyasaji wa kingono na mwanamke alifahamika kwa jina la Grace O’Marcaigh tukio lililotokea mwaka 2022.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags