Mtoto wa Angelina Jolie apata ajali

Mtoto wa Angelina Jolie apata ajali

Mtoto wa nne wa mwigizaji Angelina Jolie, Pax Jolie-Pitt, yupo chini ya uangalizi wa madaktari baada ya kupata ajali jioni ya jana Jumatatu Julai 29 wakati alipokuwa akiendesha pikipiki.

Tmz ilieleza kuwa Pax mwenye miaka 20 alipata ajali hiyo kwenye barabara ya Los Feliz Blvd kwa kugongwa na gari nyuma na kusababisha kupata majeraha kichwani.

Shuhuda wa ajali hiyo walieleza kuwa Pax alipata majeraha hayo kichwani kutokana na kutovaa kofia ya kujizuia (helment).

Pax ni mtoto wa nne kati ya watoto sita wa Angelina na mumewe Brad Pitt ambaye kwa takribani wiki sasa ameonekana akiendesha pikipiki hiyo aina ya BMX wakati wote bila ya kuvaa helment.

Licha ya mapenzi yake katika kuendesha pikipiki yaliyoshika kasi kwa siku za hivi karibuni kijana huyo pia amekuwa akiingiza sauti katika animation ya ‘Kung Fu Panda 3’ pamoja na ‘Maleficent’






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags