Mtoto mwenye uwezo wa kugeuza kichwa nyuzi 180

Mtoto mwenye uwezo wa kugeuza kichwa nyuzi 180

Ebwanaa mambo vipi? Kama kawaida hatupoi wala hatuboi katika kukusogezea habari ili uweze kujifunza na kuburudika. Basi mtu wangu wa nguvu leo na kuvusha border kutoka Tanzania hadi nchini Pakistani ambapo tunakutana na mtoto mwenye uwezo wa kugeuza kichwa chake kwa nyuzi 180.

Mtoto huyo anayefahamika kwa jina la Sameer Khan mwenye miaka 14 huko nchini Pakistani, amewashangaza watu wengi kwa uwezo alionao wa kuweza kugeuza kichwa chake kwa nyuzi 180 akisaidiwa na mikono yake, pia mtoto huyo anaweza kuzungusha mabega yake kwa nyuzi 360.

Aidha mtoto huyo amekuwa akiwashangaza watu wengi sana kutokana na viungo vyake hivyo kufanya kazi ambazo haziwezekani kwa binadamu wa kawaida.

Ni wazi kwamba mtu anapozungusha kichwa chake nyuzi 180 huweza kufa lakini hali hiyo haipo kwa mtoto huyo kutokana na uwezo alionao. Kutokana na uwezo alionao mtoto huyo kwa sasa anafanya kazi na kikundi cha dansi kiitwacho ‘Dangerous Boys’ na kumuwezesha kujipatia kipato na kuisaidia familia yake vilevile. Moja ya ndoto ya mtoto huyo ni  kuwa mwigizaji na nyota mkubwa Hollywood na Duniani kwa ujumla katika filamu za kutisha.

Dondosha comment yako hapo chini.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Habiba Mohamed

A digital journalist and writer for mwananchi scoop My stories around entertainment,fashion, Artist profile, relationship, lifestyle and career.


Latest Post