Mtoto ajiua kisa hajapata nguo za sikukuu

Mtoto ajiua kisa hajapata nguo za sikukuu

Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 13, Zamada Jafari, Mwanafunzi wa darasa la nne katika Kijiji cha Ikengwa Wilaya ya Kondoa Mkoa wa Dodoma amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia mtandio wa Mama yake chanzo kikiwa ni kukosa nguo za Sikukuu.

Tukio limetokea June 27,2023 saa 10 jioni ambapo Babu yake alijaribu kumuokoa lakini usafiri wa kumpeleka Hospitali ulikosekana hivyo alifia nyumbani na mwili wake umezikwa jana June 28,2023.

Kwa mujibu wa Ayotv ambayo ilikuwa eneo la tukio imefika Kijijini hapo kuongea na Wazazi wa Marehemu pamoja na Uongozi wa kijiji hicho ambapo Baba wa Marehemu amesema

 “Siku ya tukio nilikuwa mnadani ndipo nikapata taarifa hizi lakini Wadogo zake wanasema Dada alisema atajinyonga maana hajanunuliwa nguo za Sikukuu, ni kweli tulikubalina kwamba nitamnunulia nguo za Sikukuu lakini pesa haikutosha” alisema baba mzazi wa binti huyo

Aidha Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Ijumaa Mohamed amewaomba Wazazi pindi Mtoto anapokuwa na uhitaji na Mzazi ana uwezo basi asisite kumsikiliza ili kuwapa Watoto furaha huku akisema Watoto hawapaswi kuchukua maamuzi ya namna hiyo kwa kuwa hali ya uchumi kwa sasa ni ngumu na nguvu kubwa inaelekezwa katika chakula.

Chanzo Ayo Tv






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags