Mtoto ajipiga risasi wakati akichezea bunduki

Mtoto ajipiga risasi wakati akichezea bunduki

Mtoto mwenye umri wa miaka mitatu kutoka Miami-Dade, Florida ajipiga risasi bila kukusudia wakati akichezea bunduki aliyoikuta kwenye ‘kochi’.

Mtoto huyo alikuta bunduki ikiwa imewekwa juu ya ‘kochi’ ndipo aliichukua kwa bahati mbaya aliifyatua na kumpiga kwenye mkono wake wa kulia, kama ilivyo onekana kwenye video iliyoweza ‘kurekodiwa’ na CCTV za nyumba hiyo.

Taarifa zilizopo kwa sasa mtoto huyo anaendelea vizuri na matibabu ya mkono, lakini kwa upande wa mmiliki wa silaha hiyo ameekwa chini ya ulinzi.

Inaelezwa kuwa bunduki hiyo ni ya kijana mmoja wa familia hiyo aitwaye Orlando Young mwenye umri wa miaka 23, na kwa sasa amewekwa chini ya ulinzi kutokana na tukio hilo.

Phil Archer, Mtaalam Mashuhuri wa Usalama wa Bunduki, amesisitiza wamiliki wa silaha kuwa makini na sehemu za kutunzia silaha zao ili kuepuka madhara makubwa hasa kwa watoto.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags