Mtoto aiba gari ya baba yake na kwenda kwa mtu aliekutana nae mtandaoni

Mtoto aiba gari ya baba yake na kwenda kwa mtu aliekutana nae mtandaoni

Msichana wa miaka 12 kutoka Florida nchini Marekani na rafiki yake wa miaka 14 walifunga safari ya maili 400 kuvuka mipaka ya jimbo hilo kwa gari ambalo mtoto wa miaka 12 aliiba kutoka kwa baba yake.

Inasemekana kuwa wawili hao walikuwa wakisafiri ili kukutana na mtu waliyekutana naye mtandaoni.

Kwa mujibu wa tovuti ya habari ya NBC news  imeeleza kuwa tukio hilo limetokea siku ya Alhamisi asubuhi, na tahadhari ya kutoweka kwa watoto hao ilitumwa katika majimbo kadhaa baada ya kutoweka kutoka mji wao wa Lake Butler, Florida.

Mpaka sasa haijawekwa wazi ikiwa watoto hao walikuwa wakienda kukutana na mtu mzima au mtoto mwenzao. Inasemekana walijipeleka wenyewe kwenye mamlaka husika baada ya kujiona kwenye TV  iliokuwepo kwenye kituo cha mafuta huko Alabama kuwa wanatafutwa.

Mamlaka inasema kuna baadhi ya watu wanaotilia shaka tukio hilo linaweza kuwa la kiharifu lakini kesi hiyo sasa imekabidhiwa kwa FBI kwaajili ya uchunguzi zaidi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags