Kikitokea Kaskazini Magharibi mwa Australia zaidi ya siku 30 zilizopita, Kimbunga Freddy kina uwezekano wa kuweka rekodi ya kuwa Kimbunga kilichodumu muda mrefu zaidi
Vipimo vinaonesha kipo Pwani ya Madagascar kikiwa na kasi ya Kilometa 160 kwa saa (160km/h - 99.4mph) na kinatarajiwa kuingia Pwani ya Msumbiji kikiambatana na Mvua kubwa inayoweza kusababisha mafuriko na uharibu, baada ya hapo kitaelekea Malawi, Zimbabwe na Kusini mwa Zambia.
Shirika la hali ya Hewa Ulimwenguni WMO limebainisha kuwa linaendelea kuchambua Mfumo wa Hali ya Hewa na kukifuatilia kwa ukaribu Kimbunga Freddy.
Leave a Reply