Msechu apungua kilo 17

Msechu apungua kilo 17

Mwimbaji maarufu nchini @peter_msechu ameeleza kuwa amepungua kilo 17 ndani ya miezi sita, kutoka 144 alizokuwa nazo hapo awali.

Kupitia ukurasa wake wa #Instagram ameshusha ujumbe akieleza kupungua kwake kutoka huku akitoa shukurani kwa madaktari kwa kumpatua ushauri.

Msechu ameandika,

“Nashukuru kutoka kg 144 kwa kuwekewa puto na bila kufanya mazoezi nimetoa kilo kg 17 hadi sasa. leo ndio ilikuwa siku ya kutoa puto au kuliacha limalize Mwaka. Ahsanteni sana madkatari wangu bingwa kabisa wa #MuhimbiliMloganzila Ushauri wenu naufanyia kazi kwa ukubwa sana”

“Mwanzoni waliniambia ili Puto liwe effective kabisa unapowekewa baada ya mwezi mmoja ni muhimu ukaanza na mazoezi ya mwili ili kusaidia upunguaji wa haraka na pia kukaza ngozi inayotepeta baada ya kupoteza kilo kitu ambacho sikuweza kufanya kutokana na ufinyu wa muda niliokuwa nao nimekuja kuanza mazoezi mwezi mmoja wa mwisho kabla ya leo

“Wataalamu wangu wameona waliongezee ukubwa PUTO lililoko tumboni mwangu na sasa watalitoa mazima mwezi wa 12 (December) sasa kazi kwangu mazoezi kwa wingi jumlisha puto January navaaa uniform za chekechea”






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags