Msanii MHD aswekwa Jela miaka 12 kwa mauaji

Msanii MHD aswekwa Jela miaka 12 kwa mauaji

Mwanamuziki wa Hip-hop kutokea nchini Ufaransa #MohamedSylla maarufu kama MHD amehukumiwa kifungo cha miaka 12 jela kwa mauaji ya kijana mmoja yaliyetokea jijini Paris mwaka 2018.

Msanii huyo alikutwa na hatia ya kumuua Loic K mwenye umri wa miaka 23. katika kesi hiyo washtakiwa wengine watano nao wamehukumiwa vifungu vya kati ya miaka 10 na 18, huku wengine watatu wakiachiwa huru.

Loic K alifariki dunia Julai 5, 2018 baada ya kupigwa na kuchomwa visu na kundi la watu ambapo katika tukio hili lililo 'rekodiwa' na shuhuda MHD alionekana naye kuwepo kwenye tukio hilo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags