Mr Ibu akatwa mguu

Mr Ibu akatwa mguu

Muigizaji maarufu kutoka nchini Nigeria, Mr Ibu amekatwa mguu wake mmoja kutokana na ugonjwa unaomsumbua ambapo familia haijaweka wazi maradhi yanayo msumbua muigizaji huyo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, familia yake ili-share taarifa mpya za muigizaji huyo siku ya jana jioni ambapo walieleza kuwa Mr Ibu mpaka kufikia siku hiyo ya jana alifanyiwa upasuaji mara saba na ili kuendelea kubaki hai ilibidi akatwe mguu wake mmoja.

Aidha kupitia taarifa hiyo familia imewashukuru wanaoendelea kutoa msaada kwa ajili ya Mr Ibu huku wakisisitiza kuendelea kumchagia muigizaji huyo maana hali yake bado siyo nzuri.Mr Ibu watu wengi walimtambua kupitia movie zake kama The Collaborator akiwa na Aki na Ukwa, Mr Ibu, My Chop Money na nyingine nyingi.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudukaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags