Mtengeneza maudhui kutoka nchini Marekani Mr Beast ambaye alijulikana zaidi kupitia mitandao ya kijamii baada ya kuzikwa akiwa hai kwa siku saba, ameweka wazi kuwa anashirikiana na mabilionea nchini humo kununua mtandao wa Tiktok unaotishiwa kupigwa marufuku.
Hapo awali alionekana kufanya mzaha kwenye mitandao ya kijamii, lakini baadaye alithibitisha kuwa uwezekano huo ni wa kweli, huku akionesha baadhi ya wawekezaji katika mpango huo.
Haya yanatokea wakati serikali ya Marekani inatoa muda kwa ByteDance kuuza TikTok au kukabiliwa na marufuku ya kitaifa.
Aidha kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa zinaeleza kuwa mtandao huo unajiandaa kufunga program kwa watumiaji wa Marekani Jumapili hii, Januari 19, 2025.
Ungependa kuona nani anainunua TikTok?!
Leave a Reply