Mpango wa Cardi B kutoa albamu upo pale pale

Mpango wa Cardi B kutoa albamu upo pale pale

Baada ya kutangaza kupeleka shauri mahakamani la kudai talaka pamoja na kuweka wazi kuwa anatarajia kupata mtoto wa tatu ‘rapa’ Cardi B anaripotiwa kuendelea na mpango wake wa kutoa Album yake ya pili mwaka huu.

Kwa mujibu wa chanzao cha karibu cha mwanamuziki huyo kimeiambia tovuti ya Tmz kuwa Cardi bado anaendelea na harakati zake za kutoa albumu yake ya pili licha ya kuandamwa na majambo hayo mazito mawili.

Kama tulivyoripotiwa hapo awali, kuwa mawakili wa Cardi wamewasilisha shauri mahakamani Jumatano Julai 30, la kudai talaka kutoka kwa mumewe Offset.

Albumu ya kwanza ya Cardi ilipewa jina la ‘Gangsta Bitch Music’ ambayo ilityolewa kwa mtiririko mara mbili (Gangsta Bitch Music, Vol. 1 and 2) aliyoiachia rasmi mwaka 2016.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags