Mourinho amuwinda beki wa Man United

Mourinho amuwinda beki wa Man United

Kocha wa klabu ya Fenerbahce, Jose Mourinho ameripotiwa kuiwinda huduma ya beki wa Manchester United, Victor Lindelof ili kuimarisha kikosi chake msimu wa 2024/25.

Tovuti ya Sky Sport News imeeleza kuwa Mourinho anataka kumuona mchezaji huyo wa kimataifa ambaye ni raia wa Sweden akicheza kwenye uwanja wa Sukru Saracoglu unaomilikiwa na Fenerbahce nchini Uturuki.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 61 ambaye amepata mafanikio makubwa kama mwalimu akiwa nchini Ureno, Uingereza, Italia na Hispania, sasa anajaribu kutaka kuacha alama yake kwenye soka la Uturuki.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags