Mondi na Blue wanajambo lao

Mondi na Blue wanajambo lao

Mwanamuziki wa hip-hop Mr Blue na nyota wa muziki Diamondplatnumz wanatarajia kuachia jiwe jipya leo Januari 25.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Mondi ameweka wazi ujio wa jambo jipya kwa ku-post picha akiwa na Blue, na kuisindikiza kwa ujumbe usomekao, "Simba ft Nyani Zee, saa sita kamili usiki leo".

Mr Blue amekuwa kimya bila ya kuachia ngoma kwa miezi saba sasa, ngoma yake ya mwisho ilienda kwa jina la 'Amerudi' alimshirikisha Jux na hadi sasa inawatazamaji 91k kwenye mtandao wa YouTube. Kwa upande wa Mondi ngoma yake ya mwisho alitoa miezi miwili iliyopita iliitwa Pounds & Dollars, alimshirikisha Wouter Kellerman. Mjini YouTube inawatazamaji 1.7 milioni.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags