Mocco Genius aibukia kwenye Bongo Fleva

Mocco Genius aibukia kwenye Bongo Fleva

Jina: Idd Mohamed  (Mocco)

Birthday: 4th June

Kazi: Producer


Ebwana kama kawaida ni Ijumaa nyingine tena karibu sana kwenye segment yetu pendwa kabisa ya burudani ikiwa lengo ni kufahamu zaidi kuhusiana na wasanii chipukizi pamoja na wale ambao tayari wako mjini nini ambacho wanakifanya katika kuhakikisha wanaboresha kazi zao.

Leo bwana bila shaka jarida la Mwananchi scoop limemkamata producer makini kabisa ambaye tayari ameshafanya kazi nyingi sana kwenye tasnia ya burudani bila shaka hatokua mgeni kwako si mwingine bali ni huyu hapa kijana makini kabisa Mocco Genius.

Wengi tunamfahamu kwa jina hilo ambalo analitumia kwenye kazi zake lakini leo nitakujuza majina halisi kabisa ya bwamdogo huyo, anaitwa Iddy Mohamed Ali wenyewe wanamuita (Mocco).

Aisee ziko ngoma nyingi sana ambazo zimefanyiwa production na kijana huyu ikiwemo Sugar ya Jay Melody,Alikiba Mshumaa, Zuchu Jaro,Rayvanny Kiuno na nyingine nyingi ambazo unazifahamu.

Sambamba na hayo bwana Mocco anaproject yake mpya ambayo itaanza hivi karibuni na anaratiba ya kufanya back to back katika upande wa uimbaji lakini kwenye masuala yake ya production bado yako palepale.

Alooooh ulikua unafahamu kama Mocco anakipaji cha kuimba vilevile?kupitia mahojiano yetu na mwanadishi wa makala haya alizungumza haya juu ya suala hilo.

“Nimeingia kwenye uimbaji kwasababu hii ni karia ambayo nilikua nayo kwa muda mrefu lakini nilijitambulisha katika nyanja ya producer kwanza hivyo kwa sasa nataka watanzania wafahamu upande wangu mwingine pia”alisema.

 “Niliweka nadhiri kabisa kuwa ipo siku jamii,watanzania na dunia nzima kwa ujumla  watajua kuwa nina kipaji kingine ambacho kipo ndani yangu na sijawahi kukitumikia  ni uimbaji na wakati ndo huu ambao nimeona ni sahihi kwangu”

Licha ya kufanya vizuri kwenye masuala ya production lakini kila jatihada hazikosi milima na mabonde na hapa Mocco alikua na haya yakuzungumza.

“Kwenye production changamoto ni nyingi lakini nimeshazizoea kiasi chake kuna wakati unakutana na watu ambao wanajiona wao wakubwa kuliko ninachokifanya kwahiyo usipokua na misimamo utajikuta unafanya kazi za bure” alisema na kuongeza

“Kuna wakati unakutana na mashabiki ambao wanapenda kuimba lakini hawana vipaji vya kuimba kwahiyo unakuta unafanya kazi mara mbili kama producer, mtunzi hivyo unajikuta unafanya vitu vingi kwa wakati mmoja lakini kutatua changamoto ndiyo kutimiza lengo,” alisema.

Matarajio yake

Hata hivyo alizungumza kuhusu matarajio yake kwenye tasnia  ya burudani moja kati ya jambo ambalo alilizungumzia ni kuwa anatamani kuona wasanii wa hapa nchini wanazidi kufanya vizuri nje ya nchi.

“Nataka kusogeza muziki wangu kwenda mbele kadri inavyowezekana kutengeneza mazingira ambayo yatakuza muziki kimataifa”.alisema

Licha  ya yeye kuingia kwenye uimbaji lakini Mocco alibainisha kuwa yeye anapenda mitindo yote ya uimbaji kutokana na mashabiki kwani asilimia kubwa wanapenda kusikiliza aina zote za uimbaji.

Bila shaka utakua umeyafahamu yanayomuhusu kijana huyu lakini kuna hili hapa la msingi pia ambapo alifunga na kutueleza historia yake kwa ufupi

Historia yake

“Mimi ni mzaliwa wa kilwa lakini baada ya miaka mitatu familia yangu ilihamisha makazi bagamoyo hivyo hapo ndipo nilipokulia,nimefanikiwa kupata elimu yangu ya Msingi, Sekondari na Olevel na hapo ndipo kikomo cha elimu yangu ilipoishia.”

Sambamba na hayo alielezea vitu ambayo anavikubali kwenye maisha yake ikiwemo anapenda sana kucheza mpira wa miguu,kusikiliza muziki,kupiga vyombo vya muziki na kushiriki kwenye utunzi wa muziki.

Ukiachana na hayo ambayo anayakubali yapo pia yale ambayo hayampendi ikiwemo hapendi marafiki ambao hawaongezi kitu kwenye maisha yake yaani watu ambao hawana maarifa wala mawazo yakumpeleka kwenye mafanikio.

Ushauri wake kwa vijana

“Nawashauri vijana wenzangu tuhakikishe tunachagua marafiki ambao wanaweza kutusogeza na kutupeleka mbele hatua moja au hata mbili pia”

Kuhusu mahusiano yake

Hahaha tumefika kwenye kile kipengele chetu nyeti kabisa cha masuala ya mahusiano na hapa producer Mocco alizungumza haya.

“Kwasa hivi kiukweli siko kwenye mahusiano lakini niko natafuta mahusiano maana nimeona nipoepoe kwasababu huwa nakutana na mambo mengi unapigwa kofi la kushoto na kulia unakaa pembeni unasubiri ila nipo kwenye mazingira ya kuangalia yupi ananifaa”alisema

Aloooh mambo ndivyo yalivyo kwa upande wake itoshe kusema kwamba jimbo liko wazii hahaaha.

Mfahamu kwa ufupi kuhusu kazi zake

“Mimi nilianza production nilipotoka shule lakini wakati niko shule pia nilikua napiga bendi lakini pia madrasa nilikua nashiriki kwenye uimbaji wa kaswida na upigaji dufu pamoja na Nai.”alisema nakuongeza

“Hivyo talanta yangu huko ndiyo sehemu ambapo inmeanzia na ilikozaliwa pia nilivyokuja kwenye production nimekuja kufanya muendelezo wa kile ambacho nilikua nafanya awali hata kwenye uimbaji pia nimeanzia mbali vilevile”alisema

Hata hivyo aliongeza kwa kusema kuwa wakati anaanza kazi zake siku zote mwanzo huwa mgumu kutokana na manyanyaso na kuonekana kama hujui lakini kadri siku zilivyosogea vitu vilianza kufunguka na hadi sasa yupo akiwa anafanya vizuri kwenye game.

Ebwana eeeh kwenye hii life hakuna jambo dogo, wala jepesi usijeukafikiria kutoa ni rahisi kijana mwenzangu kaza msuli hakuana mafanikio yanayokuja tu bila kuhustle.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags