Mlinda mlango wa PSG na mkewe wavamiwa

Mlinda mlango wa PSG na mkewe wavamiwa

Golikipa wa ‘klabu’ ya Paris Saint-Germain (PSG), Gianluigi Donnarumma na mkewe wamevamiwa na watu wasiojulikana katika nyumba yao iliopo Paris usiku wa kuamkia jana Julai 20, ambapo walishushiwa kichapo na kuibiwa vito vya thamani.

Kwa mujibu wa Bbc news inaeleza kuwa mlinda mlango huyo raia wa Italia na mpenzi wake walifanikiwa kujihifadhi katika hoteli ya kifahari iliyo karibu na nyumba yao ambapo walipatiwa msaada kabla ya wawili hao kupelekwa hospitali.

Wafanyakazi wa hoteli hiyo walitoa taarifa polisi juu ya tukio hilo huku uchunguzi juu ya wizi huo ukiendelea.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags