Mkurugenzi wa ‘klabu’ alazimisha kuingia chumba cha VAR

Mkurugenzi wa ‘klabu’ alazimisha kuingia chumba cha VAR

Mkurugenzi wa ‘Klabu’ ya #Corinthians, ya Brazil, #AlessandroNunes, ameonekana kulazimisha kuingia kwenye chumba cha VAR baada ya kutoridhishwa na matokeo ya mchezo wao dhidi ya #Gremio.

Inaelezwa kuwa kipindi cha kwanza katika mchezo huo, ‘Klabu’ ya Corinthians walinyimwa mkwaju wa ‘penati’ huku wakimshuhudia ‘beki’ wao wa kati #BrunoMendez, akitolewa nje kwa kadi nyekundu.

Hali hiyo ilizua mtafaruku mkubwa na kumfanya Nunes kukata kuingia katika chumba cha Video Assistant Referee (VAR) kwa nguvu, ambapo jaribio hilo la kutaka kuingia katika chumba hicho liligonga mwamba baada ya maafisa usalama kufika eneo la tukio.

‘Mechi’ hiyo ilitamatika kwa bao 1-0 ambapo Corinthians waliibuka na ushindi.

.

.

#MwananchiScoop

#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags