Mkongwe wa soka afariki dunia

Mkongwe wa soka afariki dunia

Mkongwe wa soka nchini Ujerumani Franz Beckenbauer mwenye umri wa miaka 78 anayetambulika kama moja ya wachezaji bora kuwahi kutokea nchini humo, amefariki dunia.

Franz aliwahi kucheza katika ‘klabu’ ya #BayernMunich mechi 582 na kufikia kiwango cha juu kama mchezaji na Meneja. Pia aliwahi kushinda ubingwa wa Ulaya mwaka 1972 akiwa kama mchezaji, vilevile alishinda Ballon d’OR mara mbili.

Mwaka 1974 alishinda Kombe la Dunia akiwa nahodha wa West Germany na mwaka 1990 alinyanyua tena kombe hilo akiwa Meneja.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags