Mke wa Rais alalamika account zake kudukuliwa

Mke wa Rais alalamika account zake kudukuliwa

Taarifa kutoka nchini Nigeria ambapo mke wa Rais nchini humo, Aisha Buhari amewataka wadukuaji kuondoa taarifa za Uongo walizoweka kwenye kurasa zake za Instagram na Facebook baada ya kumdukua kwa kuwa zinapotosha Jamii.

Kupitia kusara hizo imechapishwa taarifa kuwa Benki Kuu ya Nigeria imesogeza mbele tarehe ya ukomo wa kubadili matumizi ya noti za zamani za Naira, taarifa ambayo imekanushwa na Benki

Hata hivyo Mke wa Rais Muhammadu Buhari amedai si mara ya kwanza kwa wadukuaji kuingilia Kurasa zake za Mitandao kwa lengo la kumchafua. Amesema ni jukumu la Watu wa Usalama wa Mitandao hiyo kujua nani anayefanya Mchezo huo mchafu licha ya kuwa akaunti yake inatambuliwa (tiki ya bluu).






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags