Mkahawa ambapo mauaji ya AKA yalipotokea wafungwa mazima

Mkahawa ambapo mauaji ya AKA yalipotokea wafungwa mazima

Mgahawa maarufu wa Wish unaopatikana huko Durban katika barabara ya Florida, nchini Afrika kusini umetangazwa kufungwa moja kwa moja Jumatatu ya April 10, 2023.

Haya yanajiri miezi michache baada ya rapa Kiernan "AKA" na mpishi  Tebello ‘Tibz’ Motsoane kuuawa kwa kupigwa risasi nje ya mgahawa huo.

Kupitia ukurasa rasmi wa instagram wa mgahawa huo wameshare taarifa hiyo ya kufungwa kwakwe ambayo inasomeka kama ifuatavyo

"Ni kwa huzuni mkubwa kwamba tunatangaza kufungwa kwa Wish On Florida kuanzia tarehe 10 Aprili 2023, pia tungependa kulishukuru jiji la Durban kwa usaidizi mkubwa katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, kukupa huduma wewe na nchi nzima kumekuwa na furaha kubwa na msaada wako utaandikwa kwenye urithi wa Wish On Florida."







Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags