Mjukuu wa Mandela afariki dunia kwa saratani

Mjukuu wa Mandela afariki dunia kwa saratani

 

Zoleka Mandela, ambaye ni mjukuu wa Rais wa kwanza mzalendo nchini Afrika Kusini, Nelson Mandela, amefariki dunia kwa saratani akiwa na umri wa miaka 43, familia yake imetangaza.

 

Kwa mujibu wa BBC Swahili, taarifa hiyo ambayo imeweka kwenye mtandao wa Instagram na msemaji wa familia, imeeleza kuwa Zoleka alifariki jana Jumatatu Septemba 25, 2023 jioni, akiwa amezungukwa ndugu, jamaa na marafiki.

Ripoti ya BBC imeeleza kuwa katika miaka ya hivi majuzi, Zoleka alijulikana sana kwa kuelezea matibabu yake ya saratani na pia kuwa wazi juu ya historia yake ya uraibu wa dawa za kulevya na mfadhaiko.

Si hivyo tu, lakini pia aliwekwa wazi kuhusiana na changamoto aliyoipata ya kunyanyaswa kingono wakati akiwa mdogo.

Zoleka aligundulika kuwa na saratani ya matiti, takribani miaka kumi iliyopita, na alikuwa akipata matibabu na kwamba hali yake ilizidi kuimarika, japo baadaye ilirejea.

Mwaka jana, alithibitisha kuwa alikuwa na saratani kwenye ini na mapafu, kisha ikasambaa kwa viungo vingine, na alikuwa akipata matibabu, na kwamba alilazwa Septemba 18, 2023.

BBC Swahili imenukuu maneno aliyoandika katika ukurasa wake wa Instagram mnamo Septemba 17, 2023; ambapo alieleza: “Nilifanyiwa uchunguzi wa CT scan wiki chache zilizopita, ambayo imeonyesha kuwa nina damu iliyoganda pamoja na Fibrosis kwenye pafu langu.”

“Hii inaelezea maumivu ya kifua niliyokuwa nikiyasikia. Daktari wangu wa oncologist amependekeza dawa za kupunguza damu na kemo ya

mdomo. Upande wa juu, ninashukuru sana kwamba bado ninatibika," Zoleka alieza kabla mauti haijamkuta.

.

.

Credit Mwananchi
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post