Mistari ya Jay Z kwenye kuta za maktaba kuu, New York

Mistari ya Jay Z kwenye kuta za maktaba kuu, New York

Ikiwa bongo land tunahangaika na nani atashikiria number one trending kwa muda mrefu, lakini kwa wenzetu mambo yako tofauti, Rapper Jay-Z anafanya kitu tofauti kupitia mistari yenye maneno ya kukumbukwa, na sasa mistari hiyo inasherehekewa kupitia onesho kubwa mbele ya Maktaba Kuu ya Umma mjini Brooklyn, New York (BPL).

Mistari mbalimbali kutoka kwenye nyimbo za Jay-Z, ikiwa ni pamoja na Hovi Baby, Sweet, Encore, Justify My Thug' na zingine, yalionekana kwenye mradi huu mpya.

Ina aminika kuwa kitendo hicho ni sehemu ya maadhimisho yanayoendelea ya miaka 50 ya muziki wa Hip-Hop. Huku Kampuni ya Mass Appeal imejitahidi kuendeleza jukwaa lijulikanalo kama Hip Hop 50 kwa ajili ya kusherehekea urithi wa muziki huo.

Haya kwetu bongo unadhani ni mistari ya msanii gani wa Tanzania inaweza kukumbukwa, dondosha komenti yako hapo chini mwanangu sana utueleze mtazamo wako katika hili.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post