Mike Tyson ala nyama mbichi kujiandaa na pambano

Mike Tyson ala nyama mbichi kujiandaa na pambano

Bondia wa ngumi za kulipwa kutoka Marekani, Mike Tyson ameweka wazi kuwa kwa sasa anakula nyama mbichi kwa ajili ya kujiandaa na pambano lake dhidi ya Jake Paul linalotarajiwa kufanyika Julai 2024.

Tyson ameyasema hayo wakati akiwa kwenye podcast ya ‘The Damon Elliott Show’ ambapo alieleza kuwa kwa sasa amefanya mabadiliko ya lishe na ameanza kula nyama mbichi ili iweze kumsaidia katika pambano lake na Jake.

Pambano la Tyson (58) na Jake (27) linatarajiwa kufanyika Julai 20 katika uwanja wa AT&T uliopo jijini Texas nchini Marekani pia litaoneshwa live kupitia mtandao wa Netflix.

Ikumbukwe kuwa mara ya mwisho kwa Tyson ambaye ni bingwa wa zamani wa uzito wa juu aliingia ulingoni mwaka 2020, ambapo lilikuwa ni pambano la raundi nane dhidi ya Roy Jones Jr huko Los Angeles.

Aidha kwa upande wa Jake Paul amekuwa na mafanikio kadhaa katika mchezo huo ambapo katika rekodi yake amewahi kuwashinda nyota wa zamani wa UFC kama Nate Diaz, Anderson Silva, Tyron Woodley, Andre August na Bourland.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post