Mike Tyson aahidi kumkimbiza Paul kama mwizi

Mike Tyson aahidi kumkimbiza Paul kama mwizi

Bondia wa ngumi za kulipwa kutoka Marekani Mike Tyson ameweka wazi kuwa sasa yupo tayari kwa pambano lake na Jake Paul linalotarajia kufanyika Novemba 15, 2024 kwenye Uwanja wa AT&T mjini Arlington, Texas.

Awali pambano hilo lilipangwa kufanyika Julai 20 mwaka huu huku likioneshwa live kupitia Netflix, lakini lilisitishwa kufuatia majeraha aliyoyapata Tyson wiki chache kabla ya pambano hilo.

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari Tyson amefunguka kuwa alipata majeraha lakini sasa yupo tayari kumkabili Jake paul.

“Nilikumbana na changamoto ndogo. Nilikuwa mgonjwa, lakini najisikia vizuri. Niko tayari, Yeye [Paul] anaweza kuwa amepambana na watu wengi lakini hawezi kunichapa mimi, mara tu nikimkamata huyu jamaa itakuwa imekwisha kabisa, atakimbia kama mwizi” amesema Tyson

Pambano hilo litakuwa la raundi nane, kila raundi ikiwa na dakika mbili, na wapiganaji wote wawili watavaa glavu za uzito wa 14oz badala ya glavu za 10oz.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags