Microsoft yakiuka faragha za watoto

Microsoft yakiuka faragha za watoto

Tume ya biashara ya shirikisho (Federal Trade Commission) nchini Marekani imedai kuanzia 2015 hadi 2020 Microsoft ilikusanya taarifa binafsi za watoto wa chini ya miaka 13.

Ambapo watoto hao walijiandikisha kwenye mfumo wao wa michezo ya kompyuta ya xbox bila idhini ya wazazi wao na kuendelea kuwa na taarifa hizo.

Pamoja na tuhuma hizo Microsoft ilikiuka sheria ya ulinzi wa faragha mtandaoni kwa watoto, au (coppa), hivyo italazimika kuchukua hatua kadhaa za kuimarisha ulinzi wa faragha kwa watumiaji watoto wa xbox.

Kwa mujibu wa sheria ya nchi hiyo watoa huduma za mtandaoni na tovuti zilizolenga watoto walio chini ya miaka 13 ni lazima ziwajulishe wazazi kuhusu taarifa binafsi wanazokusanya kutoka kwa watoto na kupata ridhaa yao kwajili ya matumizi ya taarifa hizo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags