Mfanyakazi wa benki aua watu watano kwa risasi

Mfanyakazi wa benki aua watu watano kwa risasi

Connor Sturgeon mwenye umri wa miaka 25 kutoka nchini Marekani, amefanya shambulio la kuua watu watano kwa risasi, huku akirusha mubashara(live) tukio hilo katika mtandao wake wa Instagram, ikiwa ni siku chache tangu ajulishwe kuwa atafukuzwa kazi.

Mtuhumiwa naye aliuawa kwa kupigwa risasi na Askari, na tayari kampuni ya mtandao huo, Meta wamefuta video ya tukio hilo lililotokea jimbo la Kentucky  na kujeruhi watu 9.

Takwimu zinaonesha kuna matukio 146 ya ufyatuaji risasi yaliyohusiha vifo vya watu wanne au zaidi Nchini Marekani kwa mwaka 2023

Kentucky ni moja ya majimbo 26 yanayoruhusu kumiliki silaha kwa mtu anayeanzia umri wa miaka 21 bila kuwa na leseni






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags