Mfahamu mwanamke mweusi wa kwanza kuwa bilionea

Mfahamu mwanamke mweusi wa kwanza kuwa bilionea

Janice Bryant Howroyd alikuwa mwanamke wa kwanza mweusi kuwa na biashara yenye thamani ya zaidi ya dola bilioni moja nchini Marekani.

Akilelewa kusini mwa nchi hiyo jimbo la North Carolina miaka ya 1950, wakati wa ubaguzi wa rangi alikumbana na matatizo mengi ikiwemo ubaguzi wa rangu akiwa anatafuta kazi hivyo basi, alitumia uzoefu wake kama muongozo alipoamua kuanzisha kampuni yake ya rasilimali watu.

Lakini kulingana na wazazi wake, maisha yake na ndugu zake wengine 10 hayangeendeshwa na ubaguzi wa rangi.

"Mama yangu na baba yangu sio kwamba walikuwa wamesoma sana, lakini walikuwa werevu mno," alisema wakati akihojiwa na kuongeza kuwa

"Walinifunza kuwa nina haki sawa kama mwingine yoyote yule, pengine sio kwa fursa zote lakini mimi ndio nilihitajika kutengeneza fursa hizo''.

Pia walinifunza nisitafute fursa hizo kwa uchungu ili hasira isiwe sehemu ya maisha yangu. Kikubwa nilichofikia ni kitaaluma na maisha yangu binafsi kutokana na kile nilichojifunza mwanzoni nyumbani, "ameongeza.

Mwaka 1976, alihamia Los Angeles, California, kufanyakazi kwa muda tu kama msaidizi wa shemeji yake Tom Noonan katika kampuni ya jarida la Billboard.

Janice anakumbuka kwamba mkuu wa kampuni alilazimika kusafiri kuhudhuria mkutano mmoja Ulaya na yeye akaachiwa fursa ya kusimamia kampuni.

"Aliporejea, alipata ofisi imebadilika sio ile alioiacha na kuiona ikiwa bora zaidi. Nakumbuka akisema nimefanya miujiza," Janice alisema.

Hapo ndipo shimeji yake alipobaini kipaji chake na kumsihi kuendelea kutimiza ndoto yake. "Tom ndio sababu ya mimi kuendeleza taaluma yangu ya ujasiriamali na nikaamua kufungua biashara," alisema Janice.

Wakati huo, sheria zinazotenganisha watu weusi na wazungu zilikuwa bado zinatumika, zilianza kutekelezwa baada ya kukomeshwa kwa utumwa.

"Nisingemuoa mume wangu na macho yake mazuri ya Buluu, wakati huo," anasema.

Sheria za ubaguzi zilipoanza kufutwa baada ya kujitokeza kwa vuguvugu za kupigania haki za raia.

Janice alikwenda kusoma katika shule ambayo ilikuwa inatekeleza mchakato wa kurejesha mambo sawa na huko ndipo alipokutana na wanafunzi wazungu katika darasa moja.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags