Mfahamu Jogoo aliyeburuzwa mahakamani kisa kuwika usiku

Mfahamu Jogoo aliyeburuzwa mahakamani kisa kuwika usiku

Jogoo mmoja nchini Ufaransa aliyepewa jina la ‘Maurice’ aliburuzwa Mahakamani kutokana na kusababisha kelele wakati wa usiku jambo ambalo lilipelekea baadhi ya majirani kukosa usingizi.

Jogoo huyo aliburuzwa katika mahakama ya mji wa Rochefort na wanafamilia waliyojulikana kwa majina Jean-Louis Biron na Joëlle Andrieux kukerwa na kelele za kuku huyo.

Katika hati iliyofikishwa Mahakamani na walalamikaji hao ilieleza kuwa katika mtaa wanaoishi kulikuwa na tulivu sana lakini tatizo lilikuwa kwa jogoo Maurice kuwa kero kwa majirani hivyo wakitaka kuku huyo kunyamazishwa.

Aidha wakati wa utetezi mmiliki wa jogoo huyo Corinne Fesseau alieleza kuwa kwa upande wake na jogoo wake hawana shida yoyote kwa majirani kwani kuku huyo alikuwa akifanya wanachokifanya jogoo wengine ‘Kuwika’.

Kesi hiyo iliyofunguliwa mwaka 2017 na kumalizika 2019 iliamuliwa kwa jogoo huyo kupewa ruksa ya kuishi katika kisiwa hicho cha Oleron huku hakimu akiwaamuru walalamikaji kulipa fidia dola 1,600 kwa mmliki wa kuku Bi Fesseau pamoja na gharama za mahakama alizotumia.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post