Mfahamu binadamu anayeongozana na kobe wake

Mfahamu binadamu anayeongozana na kobe wake

Katika ulimwengu kila binadamu huwa na chaguo lake hasa katika ufugaji ndiyo maana kuna wengine hufuga kuku, mbuzi, paka, bata na viumbe wengine.

Katika ufugaji wa aina yoyote uvumilivu huitajika ili kuweza kuendeleza aina ya mifugo ambayo mtu huimiliki, wakati wengine wakiendelea na ufugaji wa viumbe mbalimbali wa majumbani.

Fahamu kuwa yupo mtu anayeitwa Hisao Mitani ambaye yeye anafuga Kobe na mtu huyo ndiye anaaminika kuwa binadamu mvumilivu zaidi duniani.

Hisao ni raia wa Japani ambaye anamlea Kobe huyo aliyempatia jina la Bon-Chan mwenye umri wa miaka 27 sasa, alimnunua kwenye duka la kuuza wanyama, wakati Kobe huyo akiwa na umri mdogo kabisa.

Hata hivyo Hisao katika moja ya mahojiano aliyowahi kufanya alieleza kuwa anamchukulia Kobe huyo kama mtoto wake kwani hajabahatika kupata mtoto, huku akikumbushia kuwa ni mwaka wa 10 sasa tangu aanze kutembea na Kobe huyo.

Hisao amekuwa akitembea na Kobe huyo katika mitaa mbalimbali ya jiji la Tsukishima na Tokyo, huku akidai kuwa wakati mwingine hujikuta wakitembea hadi muda wa saa mbili njiani kutokana na mwendo wa kobe huyo, ambaye hutolewa kutembea mara mbili hadi tatu kwa week.

Kwa sasa Kobe huyo ana kilo zaidi ya 80 na asili yake ni Afrika, hata hivyo Hisao anadai kuwa Kobe huyo anafahamu siri zake nyingi ambazo kama angekuwa na uwezo wa kuongea basi angesema mengi.

Hisao anahesabika kama binadamu mvumilivu zaidi kutokana na uwezo wake wa kuvumilia mwendo wa Kobe wake bila kuchoka, tangu wakianza safari hadi kuimbaliza safari yao.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post