Meya Afunga Ndoa na Mamba

Meya Afunga Ndoa na Mamba

Ama kweli ukistaajabu ya mussa utayaona ya firauni, leo bwana kwenye zilizotrend mitandaoni ni kutokanana tukio la kustaajabisha limetokea huko San Pedro nchini Ufilipino ambapo Meya wa eneo hilo anayefahamika kwa jina la Victor Hugo ameoa na kufunga ndoa na mamba mwenye umri wa miaka 7.



Aidha Kabla ya tukio hilo Alhamisi ya wiki iliyopita Mamba huyo alibatizwa kwa jina la Princess, siku iliyofuata Ijumaa ndipo ndoa ikafungwa ambapo bwana hurusi alimbusu mdomoni ingawa mamba alikuwa amefungwa mdomo asije kukinukisha katikati ya sherehe na kujeruhi watu.

Bwana weeeee! Kama mnavyo jua katika kila shrerehe lazima watu waupige mpunga yaani mchele, hivyo hvyo katika harusi hiyo ya bwana Victor Watu walikula, kunywa na kusaza huku muziki ukipigwa na watu kuserebuka.

Wanakijiji hawakuishia kula na kucheza muziki tu, bali pia walipata nafasi ya kumbeba na kumshika bibi harusi huyo kwa jina la Princess na kuzunguka nae mitaani kwa furaha

Pamoja na hayo, harusi hiyo ni ya kimila, mamba anaolewa ambapo watu wa kijiji husika wanaamini kuwa ni muunganiko wa nguvu za kibinadamu na nguvu za kimungu hivyo wanaamini wavuvi maeneo yao watavua samaki wengi, watavuna mazao mengi, kupata chakula kingi, mvua nyingi kunyesha na kila aina ya neema.


Aloooooooh! Wewe huku ukiwa unamsubiri mtoto wa mama mkwe wenzako huko wanaamua kufanya maamuzi magumu, hahahah! Kijana wangu wa mwananchiscoop ukakwama wapi?






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags