Huwenda mkali wa soka na mchezaji bora katika kombe la dunia 2022, Lionel Messi akacheza tena katika kombe la dunia mwaka 2026, tofauti na alivyoashiria mwanzoni kustaafu baada ya mechi hiyo aliyoweza kuiongoza Argentina kwenye ushindi.
Kocho wa kikosi cha Agrentina, Lionel Scaloni anasema anamhitaji Messi katika kikosi chake kwa ajili ya michuano ya 2026, itakayofanyika Marekani, Canada na Mexico'
"Kwanza kabisa, tunahitaji kumwekea nafasi katika kikosi cha Kombe lijalo la Dunia 2026," alisema.
"Ikiwa anataka kuendelea kucheza, atakuwa nasi."
Hat hivyo, mara baada ya ushindi dhidi ya Ufaransa iliyoipelekea Argentina kushinda kombe la dunia katika kipindi cha miaka 36, Messi alisema kuwa hatostaafu soka la kimataifa.
"Ninafurahia kuwa katika timu ya taifa na ninataka kuendelea kwa michezo zaidi kama mabingwa wa dunia."
"Ni wazi nilitaka kustaafu baada ya ushindi huu kwa sababu hakuna kuu zaidi ya ushindi huu, “
Messi atakuwa na umri wa miaka 39 wakati wa Kombe lijalo la Dunia na alikuwa amedokeza hapo awali kwamba atastaafu baada ya kombe la dunia la mwaka huu 2022.
Leave a Reply