Messi kukutana na klabu yake ya utotoni

Messi kukutana na klabu yake ya utotoni

Mchezaji wa ‘klabu’ ya #InterMiami, #LionelMessi anatarajiwa kukutana na ‘klabu’ yake ya utotoni, #Newell’sold Boys ya #Argentine, katika ‘mechi’ ya kirafiki ya kujiandaa na msimu mpya, Inter Miami nchini Marekani Februari 15, 2024.

Messi ataungana tena na ‘klabu’ ya utotoni baada ya ‘vilabu’ vyote viwili kuthibitisha siku ya Jumatatu, Disemaba 18 kuwa watacheza ‘mechi’ ya kirafiki.

Ikumbukwe kuwa miaka sita ya Messi kuwa katika ‘timu’ ya vijana wa Newell’s Old Boys alifunga mabao 234 na kuwa sehemu ya kikosi cha vijana maarufu 'The Machine of ‘87', jina ambalo lilitokana na mwaka ulioanzishwa ‘klabu’, hiyo kabla ya kujiunga na  #Barcelona mwaka 2000.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags