Messi atumiwa ujumbe wa vitisho

Messi atumiwa ujumbe wa vitisho

Shirika la habari la AFP limeripoti kuwa mwanasoka kutoka nchini Argentina Lionel Messi ametumiwa barua ya vitisho baada ya Watu wenye silaha kushambulia duka kubwa linalomilikiwa na Familia ya Mke wake Antonela Roccuzzo jijini Rosario, nchini Argentina.

Kwa mujibu wa maelezo ya Mashuhuda wa tukio hilo lililotokea mapema jana saa tisa alfajiri, Watu wawili waliokuwa kwenye pikipiki walifyatua takriban risasi kumi na nne kwenye madirisha ya duka la Unico liliko jijini Rosario.

Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi hakuna aliyejeruhiwa katika eneo la tukio ingawa kulikuwa na uharibifu uliofanyika kwenye duka hilo huku barua ya vitisho iliachwa na ikiwa imeandikwa “Messi, tunakusubiri! Javkin ni muuza madawa ya kulevya, hatokusaidia” ambapo Javkin ndiye Meya wa jiji la Rosario nchini humo.

Aidha Meya wa Rosario Pablo Javkin ameripotiwa kufadhaika na tukio hilo huku akisema jambo hilo limeleta ongezeko la ghasia na wasiwasi jijini humo, mpaka sasa, Messi pamoja na mke wake hawajazungumzia tukio hilo mpaka sasa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags