Messi aongoza wachezaji wanaomiliki ndinga ya gharama

Messi aongoza wachezaji wanaomiliki ndinga ya gharama

Ikiwa zimepita siku chache tangu tovuti mbalimbali kuorodhesha wanasoka wanaolipwa zaidi huku CR 7 akiongoza orodha hiyo na sasa umewekwa mkeka wa nyota wa michezo ambao wanamiliki ndinga zenye gharama zaidi.

Katika orodha hiyo iliyotolewa na tovuti ya Wealth mchezaji wa ‘klabu’ ya Inter Miami Lionel Mess ndiye mchezaji namba moja anayemiliki gari lenye thamani zaidi aina ya ‘1957 Ferrari 335 Spider Scaglietti’ linaloghalimu dola 36 sawa na Sh 94.1 Bilioni.

Nafasi ya pili ikienda kwa Cristiano Ronaldo ‘Bugatti la Voiture Noire’ Sh 48.6 bilioni, Son Heung-min ‘Ferrari LaFerrari’ Sh 7.8 bilioni, John Terry ‘Ferrari 275 GTB’ Sh 5.9 bilioni, Karim Benzema ‘Bugatti Veyron 16/4 Pur Sang’ Sh 4.9 bilioni.

Akifuatiwa na Samuel Eto’o ‘Aston Martin One-77’ Sh 4.7 bilioni huku orodha ikimaliziwa na mshambuliaji Zlatan Ibrahimović ‘Ferrari Monza SP2’ Sh 4.4 bilioni.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post