Messi ajengewa sanamu

Messi ajengewa sanamu

Shirika la soko Amerika Kusini, Conmebol limemzawadia sanamu la heshima mchezaji wa timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi kwa kuingoza timu yake kushinda Kombe la dunia, mwaka jana, nchini Qatar dhidi ya Ufaransa.

Hata hivyo, nguli huyo katika soka alizawadiwa fimbo ya heshima kwa aliyoyafanya katika maisha yake ya soka, rais wa Conmebol Alejandro Dominguez alimkabidhi kwa kusema “kwa jina la mpira wa miguu wa Amerika ya Kusini na ulimwengu, leo tunakupa uongozi na amri ya mpira wa miguu duniani,” amesema Dominguez.

Aidha, kupitia ukurasa wa Instagram, mwanasoka huyo aliposti picha alizokuwa anakabidhiwa sanamu hilo na kuandika kuwa, “Asante kwa Sole Pastorutti kwa heshima hii na kwa Conmebol kwa wakati huu mzuri, ilikuwa ya kipekee sana na yenye hisia mno.” 

Sanamu hilo linatarajiwa kujengwa katika makao makuu yao karibu na sanamu la Maradona, huko Luque Paraguay. Haya kibongo bongo ungependa mchezaji gani aweze kujengewa sanamu? Dondosha komenti yako hapo chini.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags