Melody Mbassa kijana mwenye ndoto ya kuacha alama katika muziki wa dance

Melody Mbassa kijana mwenye ndoto ya kuacha alama katika muziki wa dance

It’s another weekend!! Na kama kawaida yetu lazima tukutane hapa kwaajili ya kujuzana mambo mbali mbali yanayohusiana na burudani na michezo. Leo bwana tupo na kijana ambae amaepitia mengi katika tasnia yake ya uimbaji so ungana nasi mwanzo mpaka mwisho kujua Zaidi.

Kuna baadhi ya watu wanamjua toka hapo awali, lakini kwa upande wa wenzangu na mie tulianza kumtambua kijana huyu usiku ule wa tuzo za TMA katika kipengele cha best male dance music singer of the year,  baada ya kuibuka mshindi katika kinyang’anyiro hicho.

Jina alilopewa na wazazi wake na linalo tambulika katika kitambulisho cha taifa ni Melody Felician Mbassa na lakutafutia ugali bwana anafahamika kama Melody Mbassa.

Najua kuna wengi watakuwa wanajiuliza haswa Melody ni mtu wa aina gani mwamba alieleza kuwa anatokea katika familia inayopenda muziki kwa hiyo yeye toko yuko mdogo akiwa mwenye umri wa miaka 11 mpaka hivi leo anapenda muziki na mziki ni maisha yake amesema.

Kuhusiana na historia yake ya muziki alifunguka na kueleza kuwa “Mimi nimeanza muziki nikiwa mdogo sana mwaka 2002, mwaka 2003 nikapata umaarufu kupitia na wimbo wangu ambao ulikuwa unatumika katika vipindi vya watoto wa Toto party ambao ulitamba sana miaka hiyo na kunipa umaarufu wa kufanya show ndani nan je ya nchi”alisema Melody.

Aliendelea kwa kusema kipindi hicho alikuwa mtoto wa kwanza kutoa albamu ilio kuwa na nyimbo nane ikiwemo nyimbo yake ya ‘ toto party’ ilio mpa umaarufu.

Mpaka kufikia hivi sasa amekuwa mwanamuziki mpambanaji na mapambano yake kuonekana dhahiri shahiri katika hatua ya kuwania na kupata tuzo ya mwanamuziki bora wa dance mwishoni wa mwezi wanne mwaka 2023.

Naam unavyojua raha na tamu ya mafanikio ni chungu ya changamoto kwa upande wake anaeleza kuwa changamoto anazokumbana nazo

“Changamoto kubwa ni watu kuhoji kuhusian na kijana kufanya muziki wa dance na kwanini isiwe bongo fleva hii inakuwa kama changamoto kwasababu watu wanafikiria kuwa huto wezana na muziki huo so watu wanatakiwa kujua dunia imebadilika na kila kitu kinawezekana ukitia tuu nia” amesema Mbassa

Kama inavyo eleweka kwa wakina sisi tunaotoka katika maisha ya kati tumekuwa tukipambania nafasi ambazo zitakazo fanya tutoboe moja wapo ni familia zetu kuungana na sisi kwa kile kitu tunacho fanya sio kitu rahisi.

Kwa kijana huyo yeye anamshukuru baba yake mzee Mbassa aliweza kumshika mkono mbali na vikwazo vya hapa na pale kama kuulizwa kwa nini kijana wa kileo anafanya muziki wa dance unaojulikana ni mziki wa wazee ila ameeleza kutotishwa na maswali kama hayo ata kabiliana nayo mpka afikie lengo lake alilo kusudia katika muziki wake wa dance.

Aidha jambo analofurahia ni amefanikiwa kupata elimu ya muziki na kujua kitu ambacho anakifanya kwa sababu amekuwa akiandaa muziki amabao ni kama mtu anavyo anza kujenga nyumba yake kwanzia kutengeneza msingi na ndio kama yeye anavyo fanya katika mziki huo na ndio kazi yake.

Sambamba na hayo Melody anasema kama ikitokea mtu wa kumsuppot katika muziki wake basi “Natamani zaidi mtu wa kusuppot mawazo yangu na falsafa ambazo nazifikiria muziki wangu kuufanya vizuri na tuwe na mawazo ambayo yanafanana”amesema Melody

Matamanio yake nikufanya vitu vya tofauti sana kutokana sasa hivi muziki umekuwa biashara ambayo watu wengi na wanamuziki wamekuwa wakiipambania.

Ingawa yeye amesema hana mtu wa kumuiga yaani role model anafurahia muziki wowote unao fanya vizuri kwa wale wanao chipukia na maarufu pia ila mara nyingi amekuwa anajiona mwenyewe katika muziki wake ni mtu ambae anajipa kipaumbele yeye mwenye.

Kila mtu kuna kile kitu au jambo amabalo hawezi kulisahau kabisa kwa upande wa Melody yeye ameeleza hatokuja kusahau heshima kubwa ambayo ameipata mwaka huu 29/4 mwaka huu baada ya kupokea tuzo ambazo zimemfanya ajulikane zaidi na zaidi.

Kama unavyojua kwa masanii kupata tuzo ni kama maji yamefunguliwa katika bomba mwamba huyu bwana hivi karibuni baada yta kupokea ile tuzo ameachia video yake mpya inayo tambulika kama ‘Hellena’ pia anaendelea na kufanya mwendelezo wa kutoa nyimbo mpya.

Wasanii wengi wanaokuja hapa bwana huwa lazima watuelezee wale watu au yule mtu ambae amechagiza mafanikio yake katika tasnia yake kwa upande wa Melody yeye ameeleza kuwa aliefanya afanikiwe mpaka hapo alipofikia ni baba yake mzazi ambae alimsimamia toka alipoanza muziki mnamo mwaka 2002 akiwa kama meneja wake wa muziki na ndio maana alipopata tuzo alielekeza kwa baba yake.

Kuwa baba yake ndie mtu pekee alie shikia kipaji chake tokea alipo kuwa mdogo nakusema ni moja kati ya mababa bora kuwahi kutokea kusapoti ndoto za watoto wao.

Melody akuwaacha mbali mashabiki zake kwa mchango mkubwa katika safari yake ya muziki na vyombo vya habari mbalimbli vinavyoendelea kusapoti kitu anacho kifanya .

Mwisho kabisa ndoto zake nikuacha alama katika muziki wa Kitanzania kwa mtindo wakipekee kabisa kama alivyo anza kwa kupata tuzo mbili mwaka huu na anawazia kupamabania kupata tuzo za kimataifa. Waswahili tunasema kwa mwamba huyu ni kama gari limewaka so tusiache kumsapoti na kupenda vya kwetuu.

Haya sasa mwanetu wa scoop umepata kitu hapo maana Melody ajaacha kitu kwanini isiwe na wewe kufikia hatua kama hiyo nikukumbushe tu sisi kama team scoop lengo letu ni kukujuza halafu fanial wewe ndio muamuzi eeeeee!!!, ila usiache tuu kutufuatilia katika mitandao yetu ya kijamii @Mwananchiscoop.

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags