Meli kubwa zaidi duniani imewasili Miami

Meli kubwa zaidi duniani imewasili Miami

Meli kubwa zaidi Duniani inayoitwa ‘Royal Caribbean’s Icon of the Seas’ tayari imewasili jijini Miami nchini Marekani ikitokea Finland ambapo ndipo ilipotengenezwa.

Icon of the Seas ilipokelewa na mashabiki, wadau katika bandari jijini Miami kwa lengo la kukusanya watalii ambao watasafiri kwa siku saba ndani ya meli hiyo, inayotarajiwa kuanza safari zake Januari 27, mwaka huu.

Bei ya abiria wa kima cha chini kabisa kwa mtu mmoja ikianzia $1,820 ambayo ni zaidi tsh 4 milioni, kwa siku saba Icon Seas ina jumla ya vyumba 2805 na inauwezo wa kuchukua abiria 7,600.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags